• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

DC MOYO AMEGAWA MICHE 5000 YA MINAZI NA MBEGU ZA UFUTA, CHOROKO NA MBAAZI KWA WAKULIMA WILAYANI NACHINGWEA

Imetumwa : January 23rd, 2025


Katika jitihada za kukuza kilimo nchini Tanzania, miche 5000 ya minazi na mbegu za  ufuta, choroko na mbaazi imetolewa kwa wakulima katika vijiji 15 vya Wilaya ya Nachingwea. Zoezi hili limefanyika leo, likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, katika kijiji cha Mwenge, Kata ya Mitumbati.


Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, amewashauri wakulima kuzingatia kilimo cha mazao ambayo yataweza kustahimili mabadiliko ya tabia nchi. Alisisitiza kuwa mbegu hizo zisifungiwe ndani bali zitumike ili kuleta tija kwa wakulima. Vilevile, amewaagiza maafisa ugani kuwatembelea wakulima na kuhakikisha hawakai ofisini.


Afisa Kilimo wa Wilaya ya Nachingwea, Raphael Ajetu, ametoa taarifa kuwa kuanzia mwaka 2025, zao la choroko litauzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, hatua ambayo itawawezesha wakulima kupata soko la uhakika.


Pia, kutokana na mabadiliko ya hali ya mvua, Afisa Kilimo Ajetu amesisitiza umuhimu wa wakulima kulima zao la mihogo kwa wingi katika mwaka 2025, kwani zao hili linastahimili ukame na lina umuhimu mkubwa katika kupunguza hatari ya njaa kwa wakulima wa Wilaya hiyo.


Wakazi wa kijiji cha Mitumbati, Yahaya Saidi na Salma Valence, wameishukuru Serikali kwa kuwajali katika utoaji wa miche hiyo na pia wameomba serikali kuendelea kuboresha sekta ya kilimo ili wanufaike zaidi. Wakulima ambao hawajapata miche hiyo wamehimiza juhudi za pamoja katika utunzaji wa miche ili kuhakikisha kila mmoja anafaidika. Kwa wale ambao hawajapata miche ya minazi, wanaweza kupokea mbegu za ufuta, choroko na mbaazi.


#Tupovizuri

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • VIKUNDI 55 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% WAJENGEWA UWEZO

    July 03, 2025
  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU YA FEDHA, MILIONI 649 ZAKOPESHWA AWAMU YA PILI

    July 03, 2025
  • NACHINGWEA YAJIFUNZA MBINU BORA ZA USIMAMIZI WA MIGODI KUTOKA GEITA

    June 27, 2025
  • WATUMISHI LINDI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA USHIRIKI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUJIFUNZA.

    June 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.