Tarehe 28 Julai 2025 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Hassan Moyo ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Mkoka, Marambo na Ruponda.

Akiwa Kijiji cha Mkoka, DC Moyo amekagua eneo la ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema amefurahishwa na utayari wa wananchi kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.

“Nimefarijika kuona mmeupokea mradi huu kwa mikono miwili. Tukishirikiana, utakamilika kwa wakati ifikapo Januari. Vifaa vitakavyokuja tulinde, tusiruhusu mtu yeyote kuvidokoa,” amesema DC Moyo.

Katika Kata ya Marambo, amekagua mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na matundu 12 ya vyoo katika Kijiji cha Litula, wenye thamani ya shilingi milioni 93.4.

Aidha, katika Kata ya Ruponda Kijiji cha Namanga, amekagua mradi wa ujenzi wa madarasa matano, matundu 12 ya vyoo na nyumba ya mwalimu ya familia mbili (2-in-1), mradi unaogharimu shilingi milioni 252.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.