Nachingwea, 2 Septemba 2025 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo, amefunga rasmi mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika katika Uwanja wa Sokoine, ambapo jumla ya vijana 128 wamehitimu (wanaume 108 na wanawake 20). Hata hivyo, vijana watano hawakumaliza mafunzo kutokana na utoro na kukosa uvumilivu.

Katika hotuba yake, Mhe. Moyo aliwataka vijana hao kuendeleza uzalendo kwa vitendo, kudumisha mshikamano na amani ya taifa. Aidha, aliwahimiza kuwa mabalozi wazuri katika jamii kwa kusimamia misingi ya ulinzi na usalama wa nchi.

Amesitiza kuwa Jeshi la Akiba ni nguzo muhimu ya taifa na kuwataka vijana wengine kujiunga, akibainisha kuwa uzalendo wa kweli unatakiwa kuonekana katika matendo na siyo maneno.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.