Mkuu Wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed H. Moyo May 17, 2023 amefanya ziara ya kutembelea sehemu ya mradi wa Boost iliopo Shule ya Msingi Chiwindi, Mchangani, Kaloleni na Shule ya Msingi Tunduru ya leo. Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kutembelea na kuona maendeleo ya mradi huo.
Shule ya Msingi Chiwindi Kuna ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya Elimu ya awali ya mfano na matundu 3 ya vyoo yenye thamani ya Shilingi Milioni 66.3, Shule ya Msingi Mchangani Kuna ujenzi wa madarasa 2 na matundu 3 ya vyoo wenye thamani ya Shilingi Milioni 53.1, Kaloleni Kuna ujenzi wa madarasa 2 na matundu 3 ya vyoo wenye thamani ya Shilingi Milioni 53.1 na Shule ya Msingi Tunduru ya leo Kuna ujenzi wa madarasa 2 na matundu 3 ya vyoo wenye thamani ya Shilingi Milioni 53.1.
Aidha, Mhe. Moyo ameiagiza Halmashauri kusimamia mafundi na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati na kukabidhi madarasa ya mradi huo kufikia 20/06/2023.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.