Chifu wa Kabila la Wamwera Chifu Ismail Nakotyo ametangaza kuongoza maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, tangazo hilo amelitoa alipokua katika kikao cha Wazee wa Nachingwea na Msimamizi wa Uchaguzi kilichofanyika Septemba 9, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

Katika Maombi hayo maalumu Chifu Nakotyo amewaalika viongozi wote wa dini na kimila ili ukamilisha ibada hiyo itakayofanyika katika viwanja wa Chifu Nakotyo vilivyopo nyumbani kwake Mtaa wa Boma nyuma ya Machinjio ya Wilaya.

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.