Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewasisitiza walimu na wazazi kuhakikisha watoto wanamaliza masomo yao elimu ya msingi na sekondari, amezungumza hayo leo Juni 4, 2025 katika viwanja vya shule ya msingi Majengo alipokua katika halfla ya utoaji tuzo za Elimu.
Mheshimiwa Moyo amesema kwamba katika hili ni lazima kudhibiti utoro na kudhibiti usitishwaji wa masomo kwa baadhi ya wanafunzi.
Aidha, Mheshiwa Moyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya miundombinu itakayowezesha suala zima la Elimu kama vile ujenzi wa shule za sekondari ametoa kias cha shillingi billioni 2 na ujenzi wa shule za msingi ametoa kiasi cha shillingi millioni 800.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.