Leo July 22, 2023 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo akiambatana na Mwemyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea ndugu Adinan Mpyagila na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Chionda A. Kawawa wametambulisha mradi wa maji katika vijij vitano vya kata ya Chiola.
Mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 119, mradi huu utajengwa kwenye chanzo cha mto Nyangao na utanufaisha Vijij 57 Lindi kijiji 1, Ruangwa vijiji 34 na Nachingwea Vijij 22. Kwa awamu ya kwanza unaenda kutekelezwa katika vijiji 31. Mradi unawakandarasi wawili ambao ni kampuni ya STC kwa mkataba wa Shilingi Bilioni 12 ambao wataanza kwenye eneo la kutibu maji kwenye chanzo cha Maji na EMERATE BUILDERS kwa mkataba wa ni Shilingi Bilioni 107 ambao watasambaza mabomba maeneo yote ya mradi na ameshaanza kazi.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji Vijijini (RUWASA) Mhandisi Sultani amewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huu. Pia, Mwenyekiti wa Halmashauri ndugu Adinan Mpygila amewataka wananchi wawe mstari wa mbele na wawe askari wazuri kwenye ulinzi wa vifaa na matumizi ya fedha katika mradi huo pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha hizo katika Wilaya ya Nachingwea zitakazo kwenda kupunguza taizo la Maji katika wilaya ya Nachingwea.
Aidha, Mhe. Moyo amemshukuru Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Shilingi bilioni 119 kwa ajili ya kukamilisha Mradi huo, pia ameongeza kwa kusema dhamira ya Mhe Rais ni kumtua ndoo Mama kichwani, hivyo mradi huu utakuwa mkombozi wa kutatua changamoto za maji. Amewaomba wananchi watunze mradi huo kwa umakini wa hali ya juu na wawe walinzi. Pia Mhe Moyo hajaridhishwa na hali ya barabara ya Ntimbo hivyo ametoa maagizo kwa Meneja wa TARURA atafute fedha kokote kwa ajili ya marekebisho ya barabara hiyo
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.