Wilaya ya Nachingwea haina wafugaji wengi kwakuwa toka miaka ya nyuma makabila ya maeneo haya hawakuwa na utamaduni wa ufugaji.
Mifugo iliyokuwa inafugwa ni jamii ya ndege ambao nao walikuwa wanafugwa kwa kiwango kidogo tu kwa matumizi ya nyumbani
Kwa sasa jamii ya watu wa Nachingwea wameanza kuhamasika kufuga hasa baada ya kuona matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kama RIPS,WFP,HPI na DADPS ambayo ilijishughulisha na kuhamasisha shughuli za maendeleo ikiwemo ufugaji wa ng’ombe wa maziwa,mbuzi,nguruwe na kuku
Kwa sasa wilaya ina jumla ya ng’ombe 11,273, Mbuzi 11,625, Kondoo 1409, Nguruwe 3235, Mbwa 3281 na kuku 324,200
Fursa zilizopo katika kuendeleza ufugaji:
Hali ya hewa-Hali ya hewa ni rafiki kwa ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo jambo ambalo litaruhusu uzalishaji bora wa mifugo na mazao yake
Nyanda za malisho - Wilaya ya Nachingwea ina jumla ya vijiji 25 vilivyofanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kati ya hivyo,vijiji 23 vimetenga maeneo ya malisho ya mifugo ambapo jumla ya Hekta 61,604 zimetengwa ambapo hekta 49,795.46 zenye uwezo wa kupokea ng’ombe 24,897 zilitengwa kwa ajili ya wafugaji wahamiaji katika vijiji vya Mtua,Chimbendenga,Mbondo,Kilimarondo,Kiegei B,Namatunu na Matekwe na hekta 11,808.54 ni kwa ajili ya wafugaji wa ndani kwenye maeneo mengine ya wilaya.Uwepo wa masalia ya mazao ya mashambani nao unachangia kwa kiwango cha kutosha katika kuongeza malisho ya mifugo
Uwepo wa magonjwa machache ya mifugo-Ukanda huu wa kusini una magonjwa machache sana ya mifugo ikilinganishwa na maeneo mengine jambo ambalo ni fursa adhimu katika kuendeleza sekta ya ufugaji kwa kuwa kutakuwa na ustawi wa kutosha kwa mifugo
Soko la mazao ya mifugo-Kutokana na uchache wa mifugo uliopo kwa sasa, mahitaji ya mazao ya mifugo kwa wananchi ni makubwa hivyo kuna uhakika wa soko la mazao yatokanayo na mifugo
Uzalishaji na masoko ya mazao ya mifugo:
Tasnia ya maziwa:
Aina ya mnyama
|
Waliokamuliwa
|
Uzalishaji (lita) |
Wastani wa bei kwa lita (T.shs) |
Thamani (T.shs) |
Ng’ombe
|
248 |
323,632 |
1,500 |
485,448,000 |
Mbuzi
|
0 |
0 |
0 |
0.00 |
Jumla
|
248 |
323,632 |
1,500 |
485,448,000 |
Tasnia ya nyama:
Aina ya mifugo |
Idadi chinjwa
|
Wastani wa uzitokwa mnyama (kg) |
Jumla ya kilo za Nyama |
Bei kwa kilo (T.shs) |
Thamani ya nyama(T.shs)
|
|
|
||||||
Ng’ombe
|
2,243 |
100 |
224,200 |
8,000 |
1,793,600,000 |
|
Mbuzi/
Kondoo |
71 |
12 |
852 |
9,000 |
7,668,000 |
|
Nguruwe
|
322 |
45 |
14,490 |
8,000 |
115,920,000 |
|
Jumla kuu
|
2,636 |
- |
- |
- |
1,917,188,000 |
|
Mayai:
Uzalishaji wa mayai ndani ya wilaya katika kipindi hiki unakadiriwa kuwa kama ifuatavyo:
Aina ya kuku
|
Idadi ya watagaji |
Idadi ya mayai tagwa |
Wastani wa bei/yai (TZS) |
Thamani (TZS) |
Kuku wa asili
|
112,400 |
1,686,000 |
500 |
843,000,000 |
Kuku wa mayai
|
1,740 |
628,600 |
500 |
314,300,000 |
Jumla
|
114,140 |
2,314,600 |
500 |
1,157,300,000 |
Tasnia ndogo ya uvuvi:
Changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo na uvuvi:
Halmashauri ya wilaya Nachingwea inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu ya sekta ya mifugo na uvuvi.Miongoni mwa changamoto hizo ni :
Halmashauri wakati mwingine inatumia vikundi na Redio ya Nachingwea FM katika kuelimisha wananchi juu ya masuala ya ufugaji
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.