Watanzania wamehimizwa kujenga tabia ya kupenda Kula na kunywa bidhaa za korosho kwani zina virutubisho vingi vya kupambana na magonjwa pamoja na kufanya uhamasishaji wa kuongeza thamani ya zao hilo na kuongeza pato la Taifa
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Michael Mntenjele alipokuwa akizungumza na wananchi, Wadau na wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakati WA maadhimisho ya siku ya Kula na Kunywa bidhaa zitakanazo na zao la korosho ambayo ni mahusisi kwa ajili ya uhamasishaji wa uongezaji thamani wa zao Hilo
Katika maadhimisho hayo Wananchi Wadau na wakulima wa korosho wameona bidhaa mbalimbali zitokanazo na korosho kama vile chapati, maandazi, kashata , maziwa ya korosho pamoja na mvinyo.
Amesema ulaji wa korosho licha ya kumlinda Mraji na magonjwa lakini pia usaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja Mmoja kupitia Soko la ndani na Taifa kwa Jumla
Dkt. Wilson Nene ni Mtafiti kiongozi wa zao la korosho kutoka Kituo cha utafiti tari naliendele amesema ni faraja kwao kama Taasisi kuona Matokeo ya utafiti na uhamasishaji wa Matokeo ya kilimo Katika zao hilo la korosho
Huku kaimu mkurugenzi Mkuu wa bodi ya korosho Ngangile Malegesi Akieleza mipango ya Serikali Katika kuliendeleza zao la korosho ili kuhakikisha linatumika ndani ya NCHI, kuuzika na kuongeza fedha za kigeni ni pamoja na ubanguaji wa korosho kwa asilimia 100% Katika viwanda vya ndani
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohammed Moyo Anaeleza faida za korosho kwa Afya ya binaadamu
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.