Watakaowaficha watoto wao wasipate chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kushughulikiwa
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amewataka wananchi kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi ambayo inatolewa na serikali katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kimkoa yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Mkapa Garden vilivyopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa.
“Hapa Kilwa naambiwa hali si nzuri watoto wengi hawajapata chanjo, naagiza wazazi wasiotaka kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo inayotolewa bure na serikali wachukuliwe hatua za kisheria, polisi wawakamate” Alisema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.
Aliongeza kuwa saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza kwani kwani wagonjwa waliopimwa na kupatikana na saratani asilimia 33 ni saratani ya shingo ya kizazi, na pia inaongoza kwa vifo kwani kati ya wagonjwa wanaokufa kwa saratani ya shingo ya kizazi inaua kwa asilimia 38.
Chanjo ya Saratani ya shingo ya kizazi inatolewa nchi nzima kwa watoto wenye umri wa miaka tisa hadi kumi nne.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.