Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea, Ndugu Joshua Mnyang'ali, ametoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi 76 wa uchaguzi ngazi ya kata.
Mafunzo hayo yametolewa leo agast 4, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa halmashaur ya wilaya ya Nachingwea ambapo yataendelea kwa muda wa siku tatu hadi agast 6, 2025 yakilenga kutoa elimu ya utendaji na uwajibikaji katika kusimamia ipasavyo uchaguzi kwa mujibu wa katiba, sheria kanuni na miongozo inayotoloewa na Tume huru ya uchaguzi,
Ndugu Mnyang'ali amesisitiza kuwashirikisha wadau wa Uchaguzi na vyama vya siasa kulingana malekezo na maagizo ya na Tume huru ya Uchaguzi, Pia amewasihi wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanapokea vifaa vyote na kuhakikiwa na kufikishwa katika vituo vya Uchaguzi ili kuepuka kuatiri zoezi zima la Uchanguzi,
Kwa upande mwingine wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata wamekula kiapo rasmi cha utii na kutunza siri ikiwa ni sehemu muhimu ya maandalizi kuelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025.
Aidha, amesema kuwa ni "wajibu wa kila msimamizi kuhakikisha kila hatua ya uchaguzi inafuata misingi ya usawa, uwazi na uaminifu, hivyo ni vyema kuzingatia mafunzo ili kuepukana na changamoto za uvunjifu wa amani"
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.