Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea katika mafunzo ya mikopo hiyo Bi. Rachael Lububu ambae ni Mkuu wa Divisheni ya Utumishi na Utawala, Julai 3, 2025 amewapongeza wajasiriamali hao kwa kufanikiwa kupata mikopo na kuwasihi kuzingatia matumizi bora ya fedha ili kuhakikisha malengo yanatimia.
Lububu amesema kuwa, lengo la Mheshimiwa Rais ni kuwakwamua wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kutoka katika umasikini, hivyo ni vizuri kujikita katika miradi waliyokopea na so vinginevyo.
Aidha, amewasihi wanufaika hao kutokua na uvivu katika kufanya shughuli zao kwani kwa kufanya kazi kwa bidii ndivyo itakavyosaidia kurejesha mikopo kwa wakati, katika mafunzo hayo vikundi 55 venye wanufaika zaidi ya 160 wamehudhuria na shilingi milioni 649 zimekopeshwa kwao.
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa wanufaika aliyefahamika kwa jina la Lasuli Chikawe ametoa shukrani zake kwa Halmashauri ya Nachingwea na Dokta Samia Suluhu Hassani kwa kundelea kuwakwamua wananchi kimaisha na kwa kazi nyingi anazoendelea kuzifanya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.