Mheshimiwa Diwani viti maalum kata ya Mpiruka, Veronica Makotha, alifanya mkutano muhimu katika kijiji cha Mkumba. Lengo la mkutano huo lilikuwa kuhamasisha uandikishaji katika daftari la wakazi na kuchangamkia fursa za mikopo kwa vijana.
Katika mkutano huo, Veronica aliwasisitizia vijana umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la mkazi, akisema kuwa ni hatua muhimu katika uchaguzi na katika kuomba nafasi mbalimbali za uongozi. "Siku zilibaki, tutumie fursa hii kwa uaminifu," alisema. Aliweka wazi kuwa kujiandikisha kutawasaidia vijana kutambulika katika jamii zao.
Veronica alikumbusha kwamba wanawake wamekuwa nyuma katika kujiandikisha, na akatoa wito kwao kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika uchaguzi na kugombea nafasi za uongozi. "Umefika wakati wanawake wawe daraja kwa uongozi, lazima tujiandikishe na tugombee," alisisitiza.
Mafisa maendeleo ya jamii pia walihimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuchangamkia mikopo ya 10% inayotolewa kwa lengo la kuwasaidia kiuchumi. Wananchi walionyesha ari kubwa ya kushiriki uchaguzi na fursa za mikopo, wakionesha utayari wa kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Mkutano huu umethibitisha kuwa wananchi wa Mkumba wako tayari kuchangia maendeleo yao na kuchangamkia fursa zilizopo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.