Wananchi wa watakiwa kutumia mnada wa mifugo kujipatia kipato
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Hashim Komba ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa kuanzisha mnada wa mifugo katika kijiji cha Matekwe
Ametoa pongezi hizo jana wakati akizindua mnada huo ambao umehusisha wananchi wa maeneo wilaya za Nachingwea, Masasi, Liwale na Tunduru na Nanyumbu.
Ameeleza wananchi wa tarafa ya Kilimarorondo na wilaya ya Nachingwea watanufaika kwa uwepo wa mnada huo kwa kuuza bidhaa mbalimbali kwa wananchi wanaofika mnadani hapo.
“Ni wilaya chache sana zenye minada nchini, mnada huu utawezesha kupata mapato kwa serikali ya Kijiji, Halmashaur na serikali kuu, pia watu watatumia fursa ya kuja maeneo haya kupumzika” Ameongeza Mheshimiwa Komba.
Aidha, ameitaka Halmashauri kuboresha miundombinu ya mnada huo wa mifugo kwa kuweka umeme na miundombinu mingine ili mnada huo uwe rafiki kwa wananchi wote.
Pia amewataka wananchi na viongozi wa maeneo hayo kudumisha amani kwani bila amani na utulivu hata shughuli za mnada haziwezi kufanyika vizuri.
Mapema akimkaribisha Mheshimiwa Mkuuwa Wilaya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Hassan A. Rugwa amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya uwepo wa mnada wa mifugo katika eneo hilo kwa kuleta mifugo na bidhaa zingine ili kuweza kujipatia kipato
Ameongeza kuwa ndio mnada pekee wa mifugo katika wilaya za mikoa ya kusini, hivyo amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu kwani kila kitu kitakachotakiwa kuwepo katika eneo hilo kitakuwepo ili mnada huo uweze kuwa bora zaidi
mnada huo hadi kukakamilika utagharimu shilingi 5,322,500 na utakuwa unafanyika mara mbili kwa mwezi ambapo utakuwa unafanyika kila tarehe 8 na 24kila mwezi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.