Wananchi watakiwa kulinda vyanzo vya Maji
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Rukia Muwango amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutofanya shughuli za kibinadamu
Ameyasema hayo jana kwenye kilele cha wiki ya maji ambacho kilienda sambamba na zoezi la upandaji miti kiwilaya katika kijiji cha Ruponda kata ya Ruponda.
“Wnanchi waendelee kupanda miti na kutunza mazingira, tusiishie hapa tu kila mtu akapande miti katika maeneo yake inawezekana ikawa ni miti ya matunda au miti mingine “ Aliongeza Mheshimiwa Muwango
Amewataka wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kulihi kanda miundombinu ya maji kwa kuwa wanaohujumu miundombinu hiyo wanafahamika kwakuwa wanaishi katika mazingira yao na pengine ni ndugu zao.
Aidha katika zoezi hilo amekabidhi cheti cha usajili wa jumuiya ya watumia maji wa Kijiji cha Ruponda ambapo amewapongeza kwa kupata usajili huo lakini amewataka kutoitumia jumuiya hiyo kwa manufaa binafsi
Akisoma taarifa ya Wiki ya Maji kwa Mkuu wa Wilaya Kaimu Mhandisi wa Maji Msafiri Tematema alisema kumekuwa na changamoto ya wananchi kutolinda vyanzo vya maji kitu kinachoigharimu serikali fedha ambazo zingeweza kupelekwa maeneo mengine yenye mahitaji ya huduma hiyo.
Maadhimisho ya wiki ya maji huadhimishwa kila tarehe 22 ya Mwezi Septemba ambapo huenda sambamba na zoezi la upandaji Miti.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.