Leo tarehe 22 Juni 2025, wakulima wa zao la ufuta kutoka wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale wamekubali kuuza ufuta mnada wa pili uliofanyika katika ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT), kijiji cha Mchangani, wilayani Ruangwa.
Mnada huo umeandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI ambacho kinaunganisha wakulima wa wilaya hizo tatu. Katika mnada huo, wakulima wamekubali kuuza ufuta kwa bei ya juu ya shilingi 2,710 kwa kilo, na bei ya chini ya shilingi 2,580 kwa kilo.
Jumla ya kilo 4,653,635 za zao la ufuta zimepelekwa sokoni kwenye mnada huo, ikiwa ni hatua kubwa ya kuhakikisha wakulima wanapata bei yenye tija katika msimu huu wa mauzo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.