Wafanyabiashara watakiwa kufanya kazi kwa bidii
Naibu waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Martin Manyanya amewataka wafanya biashara kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao binafsi na nchi kwa ujumla.
Akizungumza na Wafanya biashara wa mji wa Nachingwea jana katika ukumbi wa Mondlane amewataka wafanyabiashara hao kutambua biashara yeyote ina changamoto nyingi kwani ni sawa na maisha ya binadamu.
“Niwapongeze sana wafanyabiashara kwa kuacha shughuli zenu na kujitokeza kwa wingi, wizara yetu ni walezi na tunawashukuru wananchi kuitikia wito wa kuelekea katika Tanzania ya Viwanda” Alisema Mheshimiwa Manyanya
Aidha, katika risala yao kwa Naibu Waziri wafanyabiashara hao walimueleza Naibu waziri kuwa wanashindwa kufanya biashara kwa tija kutokana na uwepo wa kodi nyingi holela mfano kodi za zimamoto, kodi ya mapato isiyoendanda na wanachozalisha.
Akijibu malalamiko yao amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwani ndizo zitakazosaidia wao kupata huduma bora, amedai kuwa wafanyabiashara na serikali wanategemeana hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushirikiana mwenzie.
Naibu Waziri amefanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Nachingwea ambapo pamoja na kuongea na wafanyabiasha amekagua viwanda vya Mafuta Iulu na Kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi Famers ambavyo vyote havifanyi kazi kwa sasa
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.