Wadau wa Elimu watakiwa kutimiza wajibu wao
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimwa Godfrey Zambi amewataka wazazi, walimu, viongozi wa serikali na wadau wengine wa elimu kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuinua kiwango cha elimu kwa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika kikao cha wadau wa elimu kilichaofanyika jana katika viwanja vya Shule ya kutwa ya Nachingwea kujadili hali mbaya ya ufaulu kwa Mkoa wa Lindi
“Mkutano huu lengo ni kutafakari kwanini sisi Lindi tu ndio tunafanya vibaya, tunashindwa nini,tuna tofauti gani na hao wanaofanya vizuri, walimu wetu wana tofauti gani na wa maeneo mengine. Tutafakari kwa pamoja tunatokaje hapa” Alisisitiza Mhe Zambi
Mapema akitoa akitoa taarifa ya Mkoa, kaimu Afisa Elimu Mkoa Sondas Sondas amesema kwa miaka mitatu mfululizo Mkoa wa Lindi umekuwa ukishika nafasi za mwisho
”Kwa matokeo ya mwaka wa 2018 kati wanafunzi 6,483 ni wanafunzi 1167 ndio waliopata daraja la kwanza hadi la tatu sawa na asilimia 18” Aliongeza Sondas
Aidha wadau walioshiriki mkutano huo walitaka wadau kufikiri kwa kina namna ya kundokana na tatizo la kuwa wa mwisho kila mwaka na kuacha kulaumiana.
“Tuhakikishe mikakati iliyowekwa inatekelezwa ili tuweze kujua ni wapi kuna changamoto ili tuweze kufanya maboresho na kusonga mbele” Alisema Sostenes Gustenes
Mikutano ya wadau wadau wa elimu hufanyika kila mwaka kwa malengo ya kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.