Afisa mwandikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewasihi viongozi wa siasa kutoa ushirikiano wa dhati katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili. Hayo ameyasema leo Mei 13, 2025 alipokua katika kikao na viongozi hao.
Mhandisi Kawawa amewaambia viongozi hao kuwa ni vyema kwa kila mmoja kuhamasisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla kujitokeza kujiandikisha na kupata vitambulisho kwani zoezi hili ni la kitaifa na si chama kimoja.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ndugu Robert Mmari amesisitiza kuwa hakuna mtu atakaepiga kura kama hajajiandikisha, hivyo zoezi hili ni muhimu sana kwa wananchi wenye sifa za kupiga kura kwenda kujiandikisha, pia amesema majina ya waliojiandikisha kwa awamu ya kwanza yatabandikwa katika vituo kwa ajili ya wananchi kukagua majina yao, kufanya maboresho ya taarifa zao na pale inapobidi kuweka pingamizi kwa wananchi ambao hawana sifa za kuwa wapiga kura.
Aidha, kwa upande wao viongozi hao wamefurahi kushirikishwa katika mchakato huo na wameahidi kutoa ushirikkiano katika kila hatua yaani kuhamasisha mpaka katika uandikishaji.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.