Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa, ameeleza kuwa vijiji 20 vinakwenda kunufaika na kuhifadhi vizuri misitu ya asili ambayo uwekezaji wa biashara ya kabon wa utakwenda kufanyika katika vijiji hivyo.
Mhandisi Kawawa amesema Nachingwea imebarikiwa kuwa na eneo kubwa la miti ya asili la zaidi ya hekali 100,000 ambalo limehifadhiwa na linalindwa vizuri na ndo sababu biashara hii ya kabon na wawekezaji wa mazao mbalimbali ya misitu wanataka kuwekeza Nachingwea.
Mhadisi Kawawa ameyasema hayo alipokua katika ziara ya kujifunza biashara ya kabon na namna bora ya kuhifadhi misitu Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Tanganyika Agost, 2024.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.