Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, ameitisha kikao kazi kilichohusisha wazabuni, mafundi, wenyeviti wa vijiji, madiwani, waalimu, na watendaji. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 9 Januari katika Ukumbi wa Halmashauri kililenga kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.
Mh. Moyo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kusimamia ujenzi wa miradi ya shule mpya za msingi na sekondari, Vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu, ili wanafunzi waweze kuripoti shuleni kwa wakati. Aidha, ametoa onyo kwa wazabuni watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, akiwataka waondolewe ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, .Mhandisi Chionda Kawawa, ameagiza viongozi na wasimamizi wa miradi kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ifikapo tarehe 28 Februari 2025.
Miradi hiyo, inayotekelezwa kwa kutumia fedha za serikali na hisani, inajumuisha ujenzi wa shule na nyumba za walimu katika kata zaidi ya tano za wilaya ya Nachingwea.
Changamoto zilizobainika ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya ujenzi,
Maji, Mchanga, Kokoto na Mawe, ambazo zimechelewesha utekelezaji wa miradi. Hata hivyo, inatarajiwa kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati na kutoa faida kwa jamii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.