Jengo la OPD
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa, ametembelea kituo cha Afya Namatula ambacho kinajengwa kutokana na fedha za Tozo za miamala ya simu ambapo Nachingwea imepata Tsh Milioni Hamsini (M 250 ) . Hatua ya ujenzi; Maabara hatua ya boma umekamilika na jengo la OPD linaendela hatua ya lenta. Mhandisi Chionda ametoa maelekezo kwa fundi wa jengo la OPD kufanya marekebisho ya nguzo na kuzingatia kanuni na taratibu zote za ujenzi wa jengo .Maagizo hayo ametaka hadi kufikia siku ya Ijumaa Nov 19, 2021 yawe yameshafanyiwa marekebisho.
Mhandisi Chionda , amemuagiza Mhandisi wa wilaya kupeleka mbao kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Namatula. kwa ajili ya zoezi la kuanza upauaji kwenye jengo la maabara mapema Novemba 19, 2021 na utekelezaji wa kuanza kupaua uanze ifikapo Novemba 20, 2021 siku ya Jumamosi .
Mkurugenzi ametembelea ujenzi wa shule za msingi na Shule shikizi , ambapo alitembelea shule ya sekondari ya wasichana Nachingwea, Shule ya Sekondari Nambambo, Shule ya sekondari Namatula, Shule ya sekondari Chiola, Shule ya sekondari Mkoka, Shule shikizi Mituguru . Katika ziara hiyo , Mkurugenzi ameonesha kutoridhishwa kwa utendaji kazi wa baadhi ya maeneo na kutoa maagizo na kuahidi kutembelea tena muda wowote kwa ajili ya kuona utekelezaji wake.
Jengo la Maabara
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.