#habari
Zikiwa zimebaki siku kadhaa kufika Tarehe 23, Agosti 2022 Siku Maalum ya Sensa ya watu na Makazi ambayo itafanyika kote Nchini.
Agosti 20, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim A. Komba ( @hashim_komba )amewashukuru na kuwapongeza viongozi wa dini, Siasa na Wadau mbalimbali kwa namna ambavyo wamehamasisha na watu kuhamasika kuhusu Sensa ya watu na Makazi 2022.
" Uhamasishaji wa Sensa umefikia 99% tumalizie 1% kwa kuhesabiwa Agosti 23 ..... Hamasa na maandalizi ya Sensa yakamilike kwa kushiriki kuhesabiwa" Mhe. Komba.
Mhe. Komba ameeleza hali ya uhamasishaji na maandalizi ya Sensa kufikia 99%, na 1% iliyobaki itakamilika siku ya Tarehe 23, baada ya kuhesabiwa.
wananchi wote wanapaswa kushiriki kwani kutoshiriki Sensa ni kujinyima haki na kudhuruma.haki za wengine .
#Sautiyakomaendeleoyako
#jiandaekuhesabiwaagosti23
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.