Afisa lishe Wilaya ya Nachingwea Bi. Dalahile Zubery leo July 18, 2023 amewataka wafanya biashara wa wilaya ya Nachingwea kuzingatia kutunza chumvi sehemu kavu na zenye kivuli na sio juani, kwani chumvi hupoteza madini joto inapokaa muda mrefu juani. Chumvi ianapopoteza madini joto inapoteza umuhimu kiafya katika mwili wa binadamu Hayo ameyasema alipokua katika kikao cha Lishe cha robo ya mwisho (April - June) ya mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Nachingwea.
Aidha, Afisa Afya wa wilaya Bwana Masia amesema tayari wameandaa mkakati wa kupita katika maduka ambapo chumvi zinauzwa na kuchukua chumvi zote zitakazoonekana zimepoteza madini joto, sambamba na hilo lengo linguine ni kuwataka wafanya biashara kuhifadhi chumvi katika maeneo sahihi.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.