Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa, amesema kuwa Serikali ya Ujerumani imetoa msaada wa shilingi milioni 57.8 kwa ajili ya kufunga mfumo wa umeme wa jua katika Kituo cha Afya cha Namatula.
Ameeleza kuwa mkandarasi tayari amelipwa na kazi ya ufungaji wa mfumo huo inatarajiwa kuanza mara moja. Mfumo huo unalenga kuboresha huduma za afya hasa nyakati za usiku.
Mkurugenzi huyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufaniksha upatikanaji wa msaada huo pamoja na Serikali ya Ujerumani kwa kusaidia jitihada za halmashauri kuboresha huduma kwa wananchi wa Nachingwea
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.