Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI, kinachojumuisha Wilaya tatu za Ruangwa, Nachingwea, na Liwale, kimekabidhi vifaa tiba vya watoto njiti pamoja na wajawazito, vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 44.
Lengo la kutoa vifaa hivi ni kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kutoka maeneo yao hadi Hospitali ya Ndanda.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI, Odas Mpunga, alisema kuwa wameamua kutoa vifaa tiba ili kusaidia watoto njiti na wajawazito, kwa lengo la kurahisisha huduma na kupunguza changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.
Mpunga aliongeza kuwa RUNALI umejizatiti katika kurudisha faida kwa jamii, na hivyo wameamua kuwakabidhi vifaa tiba hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ili kupunguza adha ya wagonjwa katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo, aliwataka wauguzi na viongozi wa Hospitali ya Nachingwea kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vitatumika ipasavyo ili wananchi waweze kupata huduma bora na kupunguza usumbufu wa kutembea umbali mrefu. Pia, aliwasihi wauguzi wa hospitali hiyo kuwa na lugha nzuri na kuwahudumia wagonjwa kwa upendo na heshima.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.