Leo September 17 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya ziara katika Wilaya ya Nachingwea na kuongea na wananchi wa Wilaya hiyo katika eneo la Nachingwea Square, hii ni katika ziara yake ya kutembelea mkoa wa Lindi na Wilaya zake zote.
Mhe Rais amewaambia wakazi wa Nachingwea kuwa serikali katika kuhakikisha inarudisha kwa jamii inafanya jitihada mbalimbali za kuwaleta Wananchi wake huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na kutafuta bei nzuri na sitahiki za mazao kama ilivyo kwa mbaazi, ufuta na inategemewa na korosho itakuwa na bei nzuri. Pia, amewataka wananchi kuongeza juhudi katika kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo na serikali itaendelea kuwaletea huduma zote muhimu kama maji, Afya na Elimu.
Aidha, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa za watu kuuwawa katika kazia ya wafugaji na wakulima lakini pia kutokana na kazia za wanayama wakali (Tembo) ambao wamekua wakiharibu mazao ya wakulima na kuzuru binadamu. Mhe Rais ameahidi kwenda kuzijadili changamoto hizo kwa pamoja katika vikao vya kitaifa na kuzitafutia suluhisho kwa pamoja.
Aidha, Mhe Rais amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack kwenda kufanya ufunguzi wa ICU mpya ya kisasa iliyojengwa katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, alipanga kutembelea katika hospitali hiyo lakini kulingana na muda kutotosha ikashindiakana. Hata hivyo Dkt Samia Suluhu Hassan amevutiwa na mapokezi makubwa ya wananchi wa Nachingwea na ameahidi atarudi tena wakati mwingine.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.