Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo leo Septemba 7, 2024 amefanya uzinduzi wa Ndege Nyuki (Isiyo na Rubani) ya kisasa yenye thamani ya Sh Milioni 45 ikiwa maalumu kwa ajili ya kufukuza wanyama tembo katika maeneo yote yenye changamoto.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Kijiji cha Nambalapala kilichopo katika Kata ya Kipara Mnero Mhe. Moyo amesema zimetumika mbinu mbalimbali kupambana na tembo lakini bado wameendelea kusumbua, sasa Mheshimiwa Raisi kwa mapenzi makubwa aliyonayo ameleta ndege nyuki na kwa mara ya kwanza Tanzania imezinduliwa katika kijiji cha Nambalapala.
Ndege hiyi inabeba maji yatakayohangwa na pilipili kavu lita 30 ili iweze kuwafukuza tembo pia inauwezo wakwenda kilometa 5 na futi 400 juu, Kuna ndege nyuki ndogo ambayo kazi yake ni kuzunguka kutafuta walipo tembo ili kubwa iende kumwagia pilipili kali itakayowafanya tembo waweze kutoka kwenye maeneo walimovamia.
Aidha, kwa upande wake Afisa Uhifadhi wa TAWA ndugu Switibat Joel ametilia mkazo kwa jitihada zilizofanyika kukabiliana na tembo na ukiongeza na teknologia hii ya Ndege nyuki inaenda kupunguza kazia hii ya tembo kama sio kumaliza kabisa, pia amewataka wananchi kuchukua taadhali kwani wanyama wanaweza kuongeza ukali kutokana na teknolojia hii hivyo inapotokea askari wanafukuza tembo wafuate maelekezo yao.
Nae Diwani wa kata hiyo ya Kipara Mnero Mheshimiwa Ali Ahmad Milile ameishukuru serikali kwa jitihada inazozifanya kupambana na tembo na ni imani kubwa kwa wananchi kuwa ndege nyuki itasaidia na kuwapa nafuu.
.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.