Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dokta Grace Magembe akiambatana na wataalamu kutoka Wizara hiyo na Mkoani Lindi amefanya ziara katika Wilaya ya Nachingwea ya kutembelea hospitali ya Wilaya hiyo pamoja na kuongea na watumishi. Ziara hiyo imefanyika March 13, 2024.
Dr Magembe ametoa pongezi kwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshwaji wa miundombinu na vifaa tiba katika vituo mbalimbali vya huduma za Afya nchini ikiwemo na Hospitali ya Wilaya hiyo. Pia, Dr Magembe amewataka watoa huduma katika hospitali hiyo kuhakikisha wanatoa huduma zinazoendana na uboreshwaji uliofanyika. Ikumbukwe Hospitali ya Nachingwea ilipokea Shilingi million 900 kwa ajili ya uboreshwaji wa miundombinu.
Aidha, Dr Magembe amewapongeza Halmashauri ya Nachingwea na uongozi wa Hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya. Pia, aanatambua uwepo wa changamoto mbalimbali Katika Hospitali hiyo kama vile upungufu wa watumishi, kama wizara watalifanyia kazi.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.