Nachingwea kupatiwa gari la kubebea wagonjwa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameahidi kuipatia Halmashauri gari la wagonjwa ili kukabili changamoto zinazojitokeza kutokana na upungufu wa gari hilo.
Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati akikongea na wananchi, viongozi wa vyama vya msingi na watumishi wa Idara ya Afya alipofanya ziara kufuatilia utoaji wa huduma za Afya wilaya ya Nachingwea.
“Kutokana na maombi ya mbunge wenu na pia kwa kuwa natambua ni mchapakazi mzuri, amenieleza mna changamoto ya gari la kubebea wagonjwa nitaletea gari mpya land cruiser kwa ajili ya wagonjwa” Alisema Waziri Ummy Mwalimu
Mapema akitoa salamu za wananchi Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Masala amemueleza waziri kuwa Nachingwea ina changamoto ya gari la wagonjwa, Mashine ya X Ray na uhaba wa vituo vya afya.
Mheshimiwa Waziri Nachingwea tuna viwili tu cha afya ambapo tumepatiwa shilingi milioni 400 za ukarabati wa kituo cha Kilimarondo, ningeomba utongezee vituo hivi hasa ile zahanati ya Naipanga iwe kituo cha Afya.
Aidha Mheshimiwa Waziri ameahidi kuleta mashine mpya ya Xray na kupandisha hadhi zahanati ya Naipanga kuwa Kituo cha Afya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.