Diwani wa kata ya Mbondo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhe. Adnan Mpyagila amewataka wananchi wa kata hiyo pamoja na wananchi wote watakaonufaika na mradi wa BOOST kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mradi huo ili kufanya mradi kukamilika kwa wakati. Ameyasema April 2, 2023 alipokua katika mkutano wa jamii pamoja na kamati ya BOOST ya wilaya, mkutano umefanyika katika kjjiji cha Chimbendenga
Aidha, Ndg. Mpyagila amewkumbusha wananchi wilayani humo kwamba wanufaika wa mradi huo ni wananchi hivyo hawana budi kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.