Mwenge maalum wa Uhuru umekimbizwa wilayani Nachingwea Agosti 25, 2021 ambapo umetembelea, umekagua, umeweka jiwe la msingi na kuzindua jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya bilioni moja (1)
Mradi wa kwanza kukaguliwa na kuzinduliwa ni Mradi wa Maji Namikango wenye thamani ya Sh Milioni 315, 296,145.79 kutoka serikali kuu na sh 15,908.000.00 zimetokana na nguvu kazi kutoka kwa wananchi ambazo ni kuchimba na kufukia mitaro yenye urefu wa mita yenye urefu wa mita Elfu 7954. Mradi umewezesha upatikanaji wa huduma ya maji karibu na makazi ya watu, umepunguza muda uliokuwa unatumika katika kutafuta huduma ya maji na badala yake unatumika katika shughuli za kiuchumi, utapunguza magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama na mradi umeweza kutoa ajira kwa watu 18.
Mradi wa pili kuzinduliwa ni wa wodi ya wazazi iliyopo Hospitali ya wilaya Nachingwea iliyogharimu sh Milioni 474,946,758.00 ambapo Milioni 400,000,000.00 zimetoka serikali kuu na Milioni 74,946,758.00 zimetoka halmashauri. Manufaa ya mradi huu , unaokoa vifo vya mama na watoto ambavyo vilikuwa vinatokana na ukosefu wa mazingira bora ya kujifungulia .
Mradi wa tatu, kutembelewa ni shamba darasa ambalo limeanzishwa kwa gharama ya sh 1,232,000.00. limekuwa linatoa elimu kwa wakulimu namna bora ya kufanya kilimo cha kisasa katika mazingira ya nyumbani kwa ghrama nafuu na vifaa ambavyo vinavyopatikana nyumbani . Luteni Josphine Mwambashi amewasihii wananchi kuchangamkia fursa ya kupata elimu katika mashamba darasa yote yanayoanzishwa katika maeneo yote na kuepuka kilimo cha kizamani.
Mradi wa nne, ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi muungano kata ya Namatula yenye thamani ya sh Milioni 33, 918,000.00 ambapo Milioni Milioni 25,003,800.00 kutoka serikali kuu, Sh Milioni 1,300,000.00 kutoka kwa wadau /wahisani na Sh Laki 7,614,200.00 zimetokana na na nguvu za wananchi . Mradi huu uliwekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge Luteni Josephine Paul Mwambashi.
Mradi wa tano, kutembelea ujenzi wa shule ya sekondari Chiumbati wenye thamani ya Sh Milioni 684,237,810.00 ambapo Milioni 40,000,000.00 kutoka serikali kuu,, Milioni 516,000,000.00 kutoka halmashauri makato ya zao la korosho , na kiasi cha Sh Milioni 128, 237,810,00 zimetokana na nguvu za wananchi ikiwemo kutoa eneo lenye ukubwa wa hekta 24.42 , kuchimba msingi, na kuchimba mtaro wa maji . Kiongozi wa mbio za mwenge Luteni Josphine mwambashi amewapongeza wananchi kwa kuthamaini Elimu kuweza kutoa eneo lao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hiyo.
Mradi wa sita, uwezeshwaji watu wenye ulemavu- ujenzi wa mashine ya kukoboa na kusaga (Ufunguzi) ambaponhalmashauri imetoa sh 18,000,000.00 na kupitia asilimia 10 Halmashauri imeweza kutoa mikopo Shilingi Milioni 83,175,210.00 kwa makundi hayo. Luteni Josphine Mwambashi ameweza kuzindua mradi huo wa walemavu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.