Miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na mwenge wa uhuru ina thamani ya Tsh BILIONI 1.4, miradi hiyo ni uwezeshaji wa vijana kiuchumi wenye thamani ya Tsh Milioni 15, ujenzi wa Barabara kiwango Cha Lami Y2K Kwa Milanzi, Kwa Milanzi Hadi Voda na Polisi Kuelekea mianzini wenye thamani ya Tsh Mil 480 , ujenzi wa OPD, Maabara , Jengo la kufulia na kichomea taka vyenye thamani ya Tsh Milioni 900 , ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Majengo yenye jumla ya Tsh Milioni 80 na miradi mingine ambayo Kama vile chanzo Cha maji na uhifadhi wa Mazingira Ruponda , Shughuli za mapambano dhidi ya Rushwa na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya .
Mwenge wa Uhuru umefika wilayani Nachingwea April 16, 2023 na kuondoka kuelekea wilayani Tunduru April 17, 2023 huku kiongozi wa mbio za mwenge akiwa ni Ndg. Abdalla S. Kaim. Mwenge wa Uhuru umepitia katika miradi hiyo yote na kuridhishwa na namna miradi ilivyotekelezwa.
Asante na Karibu tena Mwenge wa uhuru wilayani NACHINGWEA.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.