Msimu ununuzi wa zao la korosho kwa mwaka 2018/2019 wazinduliwa rasmi
Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Rukia Muwango aamezindua rasmi msimu wa ukusanyaji na uuzaji wa zao la korosho kwa msimu wa mwaka 2018/2019
Uzinduzi huo umefanyika leo katika kata ya Mnero Ngongo kwa kulima kupatiwa elimu kutoka kwa wadau mbalimbali wa zao la korosho kuhusu namna zoezi hilo litakavyoendeshwa msimu huu.
Katika uzinduzi huo wakulima wametakiwa kutouza korosho zao kwa walanguzi maarufu kama chomachoma kwa kuwa kuuza korosho zao kwa wakulima ni kujihujumu wao wenyewe, na mtu yeyote atakayejihusisha na biashara hiyo atashughulikiwa.
Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewaondoa hofu wakulima kuhusu kuporomoka kwa bei kama watu wengi wanavyoongea mitaani kwani watafiti wanashuhudia kuwa korosho ya Tanzania ni bora na kubwa ukilinganisha na korosho za nchi nyingine
“Kuna uzushi kuwa bei ya korosho itashuka kwa sababu mbalimbali, lazima mtambue kuwa tupo kwenye vita ya kiuchumi , hii ni njama ya watu wabaya wasiopenda mkulima anufaike na kile anachozalisha, bei itakuwa nzuri na inaweza kuongezeka “ Aliongeza Mheshimiwa Muwango
Uzinduzi wa msimu wa zao la korosho katika Wilaya ya Nachingwea unafanyika kwa mara ya pili mfululizo ambapo kwa mwaka huu bei elekezi itakuwa shilingi 1550 na mnada wa kwanza unatarajiwa kufanyika tarehe 24.10.2018 katika ofisi mpya za RUNALI wilayani Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.