Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea Mheshimiwa Adinan Mpyagila amewataka Madiwani wote wa Halmashauri hiyo kuongeza umakini katika ukusanyaji wa mapato katika kata zao hasa katika msimu ujao wa zao la mbaazi, ameyasema hayo Leo agost 1, 2023 alipokua katika mkutano wa baraza la madiwani la robo ya mwisho ya mwaka wa frdha 2023/2024.
Mhe Mpyagila amewasihi Madiwani kuwahamasisha wananchi katika kukusanya mapato ili Halmashauri iendelee kufikia lengo la ukjsanyaji na zaidi kama ilivyokua katika mwaka wa fedha 2023/24 ambapo ilizidi malengo kwa 10%, pia amewapongeza wataalamu wa Halmashauri kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuieletea sifa Halmashauri hasa kwenye ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi.
Halmashauri ya Nachingwea imeendelea kua ni mfano wa kuigwa katika nyanja mbalimbali nchini Tanzania hivyo Mheshimiwa Mpyagila amewataka madiwani na wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha wanaendeleza miradi kama hewa ukaa na kujikita katika Uchumi wa madini kwani tayari Halmashauri ina vitalu 50, kama watafanya hivyo Halmashauri itakwenda kutegemea mapato ambayo sio ya msimu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.