Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na Vijiji wilayani Nachingwea wamepata mafunzo ya uchanguzi wa serikali za mitaa yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 27 Novemba 2024, mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Msimamizi wa Uchaguzi yamefanyika leo tarehe 30 Septemba 2024.
Msimaizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mhandisi Chionda A. Kawawa amewataka wasimamizi hao wasaidizi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuhamasisha wananchi kujiandikisha ili wawe kwenye orodha ya wapiga kura, pia amewasisitizia kuwa wanajukumu la kuwakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Katika semina hii muhimu, Msimamizi wa Uchaguzi amewakaribisha washiriki wote kushiriki kwa sababu uchaguzi huu ni fursa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na amewasisitiza kutekeleza majukumu hayo kwa kujiamini kwa ufanisi, akisema, "Tumeaminiwa kuwa tuna uwezo wa kufanya kazi hii."
Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea ndugu Robert Mmali amewataka washiriki kutoa elimu sahihi na kufuata kanuni na miongozo iliyowekwa. "Someni muelewe, na msijifanye kuwa na uelewa bila msingi. Ulizeni ili kupata majibu sahihi," .
Wasimamizi wa ngazi za Kata na Vijiji wanatarajiwa kujadili umuhimu wa uchaguzi, kuhamasisha wananchi kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali, na umuhimu wa kupiga kura kumchagua kiongozi mwenye sifa kwa ajili ya maendeleo ya jamii, amesisitiza kuwa uchaguzi huu unapaswa kufanyika katika mazingira huru, wazi, na salama.
Aidha, Mhandisi Chionda amesema watakaoonesha ufanisi katika uandikishaji na kuvuka malengo watapewa zawadi kama motisha ya kuongeza ari na ubunifu katika kazi zao.
Katika semina ya uchaguzi wa serikali za mitaa, washiriki walionesha dhamira yao ya kuendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kushiriki uchaguzi. Walisema kuwa kila mwananchi aliyefikia umri wa miaka 18 anapaswa kushiriki katika mchakato huu wa kidemokrasia.
Wakisisitiza umuhimu wa uchaguzi wa huru na haki, washiriki walikubaliana kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.