Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Ndugu Joshua Mnyang'ali, amehitimisha rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata ambapo zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashaur ya Wilaya Nachingwea leo agusti, 6 2025,
Akihitimisha mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata, Mnyang'ali amewaasa kwenda kutoa elimu sahihi kwa Makarani wa wapiga kura kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo pamoja na kuonesha kwa vitendo namna ya kutumia vifaa vya kupigia kura na kuhakikisha yanakua sawa kwa matumizi ya watu wote.
Pia, amewasisitiza wasimamizi wasaidizi hao kwa wakati huu ambapo tayari wamekua watumishi wa Tume kua na vitendo vya kiadilifu na uaminifu katika kipindi hiki kuelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025.
Aidha, Afisa Uchaguzi ndugu Robert Mmari amesema wasimamizi wamejengewa uwezo wa kuwawezesha kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo pamoja na makarani waongozaji kupitia mafunzo waliopatiwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za Tume, pamoja na kutunza rasilimali kama walivyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Uchaguzi unakua wa haki na amani,
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Naipingo Nahya Tamimu ameishukuru Tume ya Uchaguzi kwa kuwaamini na kuwapa nafasi, hivyo kwa niaba ya washiriki wengine ameahidi wataitumia kwa uaminifu na kufuata sheria na miongozo iliyowekwa na Tume ya Uchaguzi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.