• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

Moi waweka kambi Nachingwea kuwasaidia watoto wenye vichwa vikubwa

Imetumwa : April 15th, 2018

Moi waweka kambi Nachingwea kuwasaidia watoto wenye vichwa vikubwa

Jopo la madaktari kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) limeweka kambi katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ili kuwapa tiba watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Madaktari wa MOI wameweka kambi katika wilaya hiyo kutokana na kuwapo kwa idadi kubwa ya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Kambi hii ni mafanikio ya kampeni aliyoanzisha Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango.

Akizungumza wakati huduma hizo zikitolewa hospitalini hapo, Muwango, aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wenye matatizo hospitalini ili wakatibiwe.

Alisema kwamba mpaka sasa watoto 15 wameshafikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu na mpaka jana, saba walikuwa wamefanyiwa upasuaji.

“Kuna watoto wengi wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wilayani hapa na sasa kwa sababu kuna madaktari kutoka MOI, tujitokeze kwa wingi kupata matibabu,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba hospitali hiyo imekuwa ni kituo ambacho madaktari bingwa kutoka Moi wanakitumia kwa ajili ya matibabu ya wenye matatizo hayo.

Muwango alisema kampeni hiyo ya kuwasaidia na kuwafichua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, ilianza Machi Mosi na ilihitimishwa Aprili 10 kwa ajili ya kuanza matibabu ya upasuaji.

Alisema miongoni mwa sababu za kuwa na idadi kubwa ya watoto wenye matatizo hayo wilayani humo, ni watoto wa kike kuzaa wakiwa na umri mdogo.

Meneja Uhusiano na Ustawi wa Moi aliyeongozana na madaktari hao, Jumaa Almasi alisema kwamba tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara ni kubwa ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Takwimu za MOI, zinaonyesha kuwa kati ya watoto 872 waliofanyiwa upasuaji mwaka jana, theluthi moja wanatokea mikoa ya Kusini ikiwamo ya Mtwara na Lindi.

Hivi karibuni,  Almasi alikaririwa na gazeti hili akisema kwamba kati ya watoto 19 waliofanyiwa upasuaji katika siku za karibuni, 10 walitokea kwenye mikoa hiyo na tisa katika mikoa mingine nchini.

Mmoja wa wazazi ambao mtoto wake amepata matibabu, Rahel Mhagama kutoka katika Kijiji cha Mgazini, Songea alisema kwamba upatikanaji wa huduma hizo katika Hospitali ya Nachingwea umeleta nafuu kwani awali, alishauriwa ampeleke mtoto wao Hospitali ya Muhimbili. (Chanzo: Gazeti la Mwananchi )

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANAFUNZI WA NACHINGWEA HIGH NA RUGWA BOYS WAAGWA KWA HAFLA FUPI, WAJIANDAA KWA MITIHANI YA TAIFA

    April 26, 2025
  • SDA NA LIIKE WATOA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA KWA MANGALIBA NA WALOMBO KWA AJILI YA KUIMARISHA UTAMADUNI SALAMA

    April 28, 2025
  • DED NACHINGWEA : AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA VIWANGO

    April 09, 2025
  • RC LINDI : MIRADI YOTE ITAKAYOPITIWA NA MWENGE IZINGATIE MATUMIZI BORA YA FEDHA

    April 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.