Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhe. Adinani Mpyagila amemkabidhi rasmi eneo la ujenzi (Site ) mkandarasi ambaye ni Corporation Sole Works Superintendent (Vikosi vya ujenzi ) iliyo chini ya wizara ya ujenzi Leo April 5, 2023 .
Mhe. Mpyagila , wakati akikabidhi eneo hilo ameitaka kampuni ya ujenzi kuhakikisha ujenzi unazingatia viwango na muda uliowekwa kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi unavyyosema .
" Tunatamani kuona ujenzi wa ofisi hii unakamilika ndani ya miaka miwili " Mhe. Mpyagila .
Aidha, amewasihii wananchi kutambua eneo la ujenzi wa ofisi hiyo ambalo lipo kata ya Nangowe umetokana na mchakato wa vikao kadhaa vilivyoshirikisha waheshimiwa madiwani na ushauri kutoka kwa wataalamu , hivyo eneo hilo limekidhi vigezo vyote hasa ukubwa .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Longnus Nambole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi ndani ya Wilaya zikiwemo za ujenzi wa ofisi hiyo ya Halmashauri ambapo awamu ya kwanza zaidi ya Bil 1 zimeletwa. Ametoa wito kwa mkandarasi Kujenga kwa kuzingatia ubora unaohitajika.
Naye Katibu wa mbunge Ndugu George Martin kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Amandus Chinguile , amesema wananchi wanatamani kuona jengo linakamilika ili liweze kutumika kwa wakati hivyo Kama mkandarasi atapata changamoto yoyote asisite kuiona ofisi ya Mbunge kwa utatuzi wa changamoto kwa wakati .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.