Mkuu wa wilaya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo ameagiza kufanyike upimaji katika maeneo tofautitofauti katika vijiji vya Kata ya Ruponda ili kuapa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata.
Mheshimiwa Moyo ametoa maagizo hayo ili kuhakikisha eneo lenye vigezo ilinapatikana kwa kuwashilikisha wananchi wa kila kijiji katika kata hiyo, pia amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwashirikisha kikamilifu wananchi kunapotokea fursa na masuala ya maendeleo katika maeneo yao ili kuepusha migogoro itokanayo na kukosekana kwa taarifa.
Aidha, Mheshimiwa Moyo amewaagiza wataalamu kutoka Ardhi na Ujenzi kukagua maeneo yote yaliyopendekezwa na kuharakisha mchakato huo ili kupata eneo lenye vigezo na kuanza ujenzi mara moja.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.