Hospitali ya wilaya ya Nachingwea imepokea vifaa tiba vya kisasa vya ICU vyenye gharama ya zaidi millioni 383 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa watakao na hali mbaya zaidi.
Akizungumza wakati wa kukagua vifaa hivyo,mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa vifaa tiba hivyo vimegharimu zaidi ya Milioni 385 kununulia vifaa hivyo.
Moyo alisema kuwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan anahakikisha kuwa kila wilaya ikuwa na huduma bora za afya ili kuwawezesha watanzania kufanya kazi bila kuhofia kuhusu huduma za afya.
Alisema kuwa jengo la ICU ya Hospitali ya wilaya ya Nachingwea ndio jengo bora kuliko majengo yote Tanzania hivyo limekuwa mfano wa kuigwa kwa ujenzi bora uliojengwa.
Moyo alisema kuwa jengo hilo limetumia kiasi cha shilingi millioni 250 fedha kutoka serikali kuu na kuwaomba watumishi wa Hospitali hiyo kuvitunza vifaa hivyo pamoja na jengo hilo la ICU kwa faida ya watanzania.
Alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi na vifaa tiba vya ICU ya Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.