Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa March 06, 2025 amegawa mitungi ya gesi kwa zaidi ya wanawake 3000 ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais za matumizi ya nishati safi na utunzaji wa Mazingira.
Mitungi hiyo imeuzwa kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 19,500 ambako wanawake hao wamechangia kiasi hicho cha fedha na tayari zaidi ya Milion 40 zimeshakusanywa na kulipwa kwa kampuni ya Taifa Gas kwa ajili ya kuwapa wanawake hao.
Kuelekea siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 ya mwezi March kila mwaka kumefanyika makongamano mbalimbali nchini ambapo leo March 6, 2025 ni zamu ya kongamano hilo la kanda ya kisini linalofanyika Wilayani Nachingwea katika Viwanja vya Maegesho ya malori.
Moja katika ya mada kubwa katika makongomano haya ni Matumizi ya nishati safi na utunzaji wa Mazingira.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.