• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

MHE. DKT. JAFO AKOSHWA NA UBORA WA NANE NANE KANDA YA KUSINI NGONGO.

Imetumwa : August 8th, 2025

Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara  amefurahishwa na maandalizi na ubora wa viwanja vya maonesho ya Nane nane Kanda ya Kusini, vilivyopo Ngongo, Mkoani Lindi.

Pongezi hizo amezitoa akihutubia wananchi wakati wa kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika tarehe 8 Agosti 2025, Mhe. Jafo ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesifu kwa dhati juhudi za mikoa ya Lindi na Mtwara katika kuhakikisha viwanja hivyo vinakuwa vya kisasa, vyenye miundombinu bora ikiwemo barabara za lami, hali inayochochea ubora wa viwanja hivyo.

“Mmeweka alama ya kipekee kwa kuandaa viwanja vyenye hadhi na vigezo bora kwa maonesho haya. Hii ni hatua muhimu katika kutangaza fursa na kuhamasisha uendelezaji wa sekta ya kilimo na uchumi wa viwanda,” amesema Mhe. Jafo.

Katika hotuba yake, Mhe Jafo pia amezipongeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, akibainisha kuwa mikopo hiyo imekuwa kichocheo kikubwa katika kuimarisha biashara ndogondogo, shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.


Akizungumzia juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jafo ameeleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 626 zimetolewa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo za kilimo, ambapo zaidi ya asilimia 85 ya pembejeo hizo zimeelekezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, hususan kwa mazao ya kimkakati kama korosho.


Aidha, amewataka wananchi wa Kanda ya Kusini kutumia maarifa na teknolojia walizojifunza kupitia maonesho haya ya nane nane ili kuongeza tija katika uzalishaji, kuongeza kipato na kuchangia ustawi wa jamii.


Kauli mbiu ya Maonesho ya Nane nane  ni “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NACHINGWEA KUPITIA CHAMA CHA MAKINI

    August 23, 2025
  • TAASISI ZAIDI YA 60 KUKUTANA PAMOJA OCTOBA NA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI.

    August 29, 2025
  • ELIMU YA WATU WAZIMA ICHANGAMKIWE ILI KUEPUKA MAADUI WATATU

    August 22, 2025
  • DEO SEC : KUTOKA MEMKWA KWENDA CHUO KIKUU INAWEZEKANA, TUHAMASISHE NDUGU ZETU KUJIUNGA NA ELIMU YA WATU WAZIMA

    August 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.