Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Bi. Misoji Sahani amewataka wakazi wa kijiji cha Kiegei A kilichopo kata ya Kiegei na kijiji cha Chimbendenga kilichopo kata ya Mbondo kujitolea kwa hali na mali katika utekelezaji wa miradi iliyoletwa katika maeneo yao. Hayo ameyasema April 2, 2023 alipotembelea vijiji hivyo kama mjumbe wa kamati ya Mradi wa BOOST wilayani humo.
Aidha, Bi. Sahani amewasihi wakazi hao kuwa kwa kujitolea kuna uwezekano wa kubakiza fedha na zikasaidia kukamilisha miundombinu mingine katika miradi hiyo. Pia, Mhandisi amewashauri vijana kujifunza shughuli mbalimbali kupitia miradi hii ili waweze kupata ujuzi utakaoweza kuwaingizia kipato.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.