Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe, Deus Sangu amepongeza mfumo wa kutoa huduma kwa wananchi kwanjia jumuishi unaojulikana kama One Stop Centre uliotumika kwa mara ya kwanza Halmashauri ya Nachingwea ukizikutanisha Taasisi mbalimbali sehemu moja na kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Sangu ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kupata maelezo ya namna ambavyo Halmashauri za Mkoa wa wa lindi unavyotumia mifumo mbalimbali katika kuwahudumia wananchi ukiwemo wa kadi-Alama, One Stop Centre, Mfumo wa utunzaji Mazingira na Mfumo wa ndani wa upimaji utendaji wa kazi.
Aidha, amesisitiza matumizi ya mfumo wa One Stop Centre kutumika katika Halmashauri zingine kwani lengo la Serikali na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona wananchi wanafikiwa na huduma pale walipo.
Mhe. Sangu aliambatana na katibu Mkuu-Utumishi Ndugu Juma Mkomi .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.