Leo, Machi 5, 2025, Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na Maafisa kutoka Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii, wameendesha mjadala wa kijamii na mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia na afya ya uzazi kwa makundi ya vijana,viongozi wa kijamii, watu mashuhuri na wazazi katika Kata ya Mpiruka, wilayani Nachingwea. Majadiliano na Mafunzo haya yalilenga kuongeza ufahamu na kukuza ulinzi dhidi ya ukatili wa kijinsia,huduma rafiki za afya kwa vijana, kubainisha Mila na desturi kandamizi pamoja na kusisitiza umuhimu wa haki za wanawake na wasichana.
Ndg. Denice Simeo, Afisa Vijana wa Shirika la Marie Stopes, aliwataka vijana kutumia maarifa waliyojifunza ili kuwa mabalozi wazuri katika kupinga ukatili wa kijinsia na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Aliwahimiza pia kushiriki kwa wingi katika kongamano la wanawake litakalofanyika kesho, Machi 6, 2025, ambalo Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na kuwa sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi 2025.
Washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kwa elimu waliyoipata na kuahidi kuwa wajumbe wazuri katika kupinga ukatili wa kijinsia na kuchangia katika kujenga jamii yenye usawa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.