Habari Picha:
Nachingwea jogging inaendelea kuwa hamasa kubwa kwa jamii, ambapo wakazi wa mji huu wanashiriki mazoezi ya kawaida katika viwanja vya Sababa. Hii ni fursa nzuri ya kuimarisha afya ya mwili na akili, huku wakifanya jogging pamoja na michezo mingine ili kudumisha ustawi wa jamii.
Mazoezi haya ya kila mara yanasaidia kupunguza hatari ya magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo. Tushirikiane kwa pamoja katika harakati hizi za kukuza afya bora na kuimarisha umoja katika jamii yetu.
Jiunge na Nachingwea Jogging -afya bora, nguvu zaidi!
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.