March 06, 2024 yamefanyika Maadhimisho ya siku ya Wanawake wilaya ya Nachingwea katika Kijiji cha Nditi kwenye uwanja wa shule ya Msingi. Ambayo kidunia yanadhimishwa March 8 kila mwaka, maadhimisho hayo yameambatana na zoezi la kukabidhi chakula na bidhaa mbalimbali kwa familia zilizoathiriwa na Tembo hususani wanafunzi.
Maadhimisho hayo yameandaliwa na kufanikishwa na kamati ya wanawake wapenda maendeleo kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya jamii ya Halmashauri ya Nachingwea ambapo hao awali February 26, 2024 walifanya harambee katika ukumbi wa Mondulane Mess na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Nachingwea na nje ya Nachingwea walioguswa na Kadhia ya iliyowapata wakazi wa kata ya Ngunichile na kata ya Nditi.
Katika maadhimisho hayo Mahindi gunia 20, Maroba ya nguo ,Viatu Mbaazi gunia 1,Mashati 119, Majora ya vitambaa kwa ajili ya sare za shule, Daftari Katoni 6,Kaunta buku 39, Peni box 3 ,Penseli box 8,Kiloba cha unga kg 10 pamoja na taulo za kike box 10 zimetolewa kwa wakazi na wanafunzi wa Nditi na Ngunichile.
Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Mohamed Moyo Mkuu amewapongeza sana wanawake wapenda maendeleo kwa kazi kubwa waliyoifanya na Moyo na upendo waliouonesha kwa Wananditi na Ngunichile pamoja na wadau wote waliochangia.
Aidha, amewataka wazazi wa Nachingwea kuwekeza nguvu kubwa katika kumuinua mtoto wa kike na kuwataka kuacha tabia ya kuozesha watoto wakiwa na umri mdogo na kuwataka wajifelishe mtihani na kuwapeleka kwenye kazi za ndani. Pia, Mhe Moyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi waserikali za mitaa.
#tukivizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.