Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Februari 19, 2025 katika Viwanja wa Madini wilayani Ruangwa.
Mhe Majaliwa amesema lengo la kampeni hii ni kuongeza haki na kuwatambulisha wananchi ubunifu uliofanywa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan wa utaratibu wa kuwafikishia wananchi wasio na uwezo wa kujipatia huduma za misaada ya kisheria misaada ya kisheria bure.
Kampeni hii ilizinduliwa mnamo mwezi March 21, 2024 na Lindi ni Mkoa wa 19 tangu kuzinduliwa kwakampeni hiyo,
wadau wamekua na mchango mkubwa katika kuhakikisha kampeni hii inawasaidia wananchi bila gharama, pia ametoa shukrani na pongezi kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa utawala bora na wenye maono ya mbali unaowanufaisha Watanzania, Rais anafahamu shida na kero za wananchi wenye kipato cha chini katika masuala ya kisheria na akaanzisha kampeni hii.
Kampeni hii imeleta matokeo mazuri kwani wananchi mbalimbali katika kila Mkoa ambako kampeni hii imepita wamepata na wanaendelea kupata haki zao kwani tangu kuzindualiwa kwa kampeni hii March 21, 2024 huduma hii imewafikia jumla ya wanachi 1,373,099 na miongoni mwa wanufaika wa Kampeni hii ni watoto, wanafunzi na wajane na imetatua kero mbalimbali katika kesi mbalimbali za mirasi kwa wananchi 5ambao walipokonywa haki zao
Aidha, Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha haki za wananchi zinapatikana kulingana na sheria husika kwani hasa ndio lengo la Dokta Samia na serikali ina mpango wa kuajiri wanasheria wapya 500 na kuwatawanya katika kila halmashauri
Huduma hizi zitatolewa siku 9 mfululizo kuanzia February 20 hadi 28 katika ngazi ya wilaya kata na vijiji huku zikienda na kauli mbiu isemayo
Haki, Usawa, Amani na Maendeleo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.