Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa amewataka watendaji wa kata zote za Halmashauri hiyo kuhakikisha wanakusanya na kupelekeja taarifa sahihi za lishe kwa wataalamu wa lishe, pia ameagiza maafisa Elimu Kata wote kushirikiana kwa karibu na watendaji ili kupata taarifa zilizo sahihi za wanafunzi wanaokula shuleni na wasiokula. Mhandisi Chionda ameyasema hayo Julai 18, 2023 alipokua katika kikao cha Lishe cha Robo ya mwisho (April – June) ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Mhandisi Chionda amewakumbusha watendaji kutosubiri vikao ili wakumbushwe kuhusu lishe bali kila mmoja wao aipe kipaumbele na kufanya utekelezaji wa kukusanya taarifa kwa wakati. Amewasissitiza watendaji kuendelea kusimamia ratiba za maadhimisho ya siku ya lishe kikamilifu ili kuhakikisha kila kijiji kinafanya maadhimisho hayo. Mhandisi Chionda pia amewataka wataalamu wa lishe kushindanisha kata katika ukusanyaji wa taarifa za lishe ili kutoa motisha, yeye kama Mkurugenzi atatoa motisha kwa kata 10 zitakazofanya vizuri.
Aidha, Mhandisi Chionda na Dokta Ramadhan Maige ambae ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea kwa pamoja wamewataka wataalam wa afya kushuka mpaka kwenye jamii na kuipa jamii Elimu juu ya lishe ili waweze kufahamu umuhimu wake na kuipa kipaumbele.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.